9 Machi 2015 - 21:00
Mafuta ya Libya yaingia mikononi mwa magaidi

Katika muendelezo wa mapambano ya ndani ya Libya kikundi kimoja cha kigaidi kimefanikiwa kuiteka moja kati ya sehemu muhimu za mafuta nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: siku ya Jumamosi kundi moja la kigaidi ambacho mpaka sasa hakija jitambulisha kwa jina maalumu kimefanya mashambulizi makali na jishi la nchi hiyo hata kufanikiwa kuiteka moja ya sehemu muhimu za kuchimba mafuta iitwayo Almabruk katika mji wa Sitra nchini humo
Katika mashambulizi hayo watu 10 kati ya wanajeshi wanaorinda sehemu hiyo wamepoteza maisha ambapo 4 kati yao wamekufa kutokana na athari ya mashambulizi hayo na wenginio sita waliwanyonga baada ya kuiteka sehemu hiyo.
Sehemu hiyo yakuchimba mafuta nikatika sehemu muhimu za uzalishaji wa mafuta nchini Libya ambapo shirika moja la ufaransa limeweka hisa katika kuchimba mafuta ya sehemu hiyo.